A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 16, 2019

Shambulio la kigaidi Kenya laua watu 14


Hadi sasa inaripotiwa kuwa takribani watu 14 wameuawa na watu wenye silaha waliotambulika kutoka kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab, ambao walivamia eneo la ofisi la 14 Riveside, Nairobi Kenya.

Miongoni mwa maOfisa wa Marekani aliuambia mtandao wa Reuters kuwa miongoni mwa watu hao waliouawa, mmoja ni raia wa Marekani.

"Tunathibitisha kwamba raia mmoja wa Marekani ameuawa katika shambulio hili", amesema Ofisa huyo bila kueleza zaidi taarifa zaidi juu ya tukio hilo.

Utakumbuka kuwa nchi ya Kenya imekuwa ikivamiwa ikilengwa na kundi la Al Shabaab tangu mwaka 2013, ambapo ilivamia jengo la kibiashara la Westgate Jijini Nairobi na kuua watu 67.

Shambulio la 4 Riveside lilitokea hapo jana ambapo makundi ya wafanyakazi wapatao 150 walikuwa wakisindikizwa kwaajili ya kupata hifadhi na wengine wengi wakisalia ndani wakipewa huduma ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages