Bondia wa kiphilipino Manny Pacquiao amefanikiwa kutetea Ubingwa wake wa Dunia wa Boxing Welterweight kwa kumpiga kwa point bondia Andrien Broner na Las Vegas Marekani na kuutetea Ubingwa wake wa mkanda wa WBA Welterweight.
Manny Pacquiao ambaye ni Bingwa mara 70 amedhiirisha kuwa umri ni namba tu kufuatia kupigana pambano lake la kwanza toka atimize miaka 40, wakati Adrien akiwa kazidiwa miaka 11 na Pacquiao, pambano hili Floyd Mayweather pia alilifuatilia.
Andrien aliingia ulingoni kupigana na Pacquiao akiwa na uzito sawa (welterweight) ila umri akiwa na umri wa miaka 29, tofauti ya miaka 11 kati yake na Pacquia, pambano hilo lilichezwa MGM Grand na kuhudhuriwa na watu zaidi ya elfu 13, baada ya pambano Pacquiao aliomba kumtaka Mayweather arudi ulingoni yupo tayari kupambana nae.
No comments:
Post a Comment