A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, August 18, 2018

DC awapiga "STOP" wavamizi


Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufuata sheria na kuacha uvamizi wa maeneo ya watu ili kupunguza migogoro isiyo yalazima.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Msongola Mjema amesema hakuna mwananchi anayerusiwa kujichukulia sheria mkononi kwa kujenga nyumba katika kiwanja au shamba lamtu kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

"Wananchi nataka niwaambie kuwa mashamba hayo yanamilikiwa na watu, ikiwa mwenye kiwanja au shamba atatoa taarifa kuhusu uvamizi na wewe uliyejenga huna hati na yeye ndiye mwenye hati tutavunja nyumba yako hatakama umetumia pesa kiasi gani" amesema.

Aidha Mjema ambaye anaendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi ametembelea mradi wa maji Kitonga na zahati katika eneo Luhanga  na kushauri na kusisita watu kuwa na matumizi Mazuri ya pesa za serikali katika ujenzi wa miradi .

Kwa upande wao wananchi wa kata ya Kitonga wametoa kero zao huku kero kubwa  zikiwa ni umeme, barabara, Maji, Afya, na Elimu, ambapo zote zimejibiwa na kuaahidi kuwa Serikali imezichukua changamoto zote nyingine zishaaanza kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages