A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, August 6, 2018

BAADHI YA VIONGOZI WA CHADEMA WAHAMIA CCM

Aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingungiti  kupitia chama cha CHADEMA Omary Kumbilamoto (Kulia) akizungumza na wanachana wa CCM baada ya kujiunga na chama hicho hivi karibuni  wakati wa Mkutano wa ndani wakuwakaribisha wanachawaliojiunga na chama hicho 


Baadhi ya wanachama hao walitambulisha na uongozi wa CCM Wilaya ya Ilala ni pamoja aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mwita Waitara, Naibu Meya Manispaa ya Ilal na Diwani Kata ya Vingungiti Omary kumbilamoto pamoja na  Mwenyekiti cha CHADEMA Mkoani Mtwara.



Wanachana wengine ni baadhi ya Wenyeviti wa  Serikali za Mitaa katika Jimbo la Ukonga, pamoja na wanachama wa CHADEMA ambao wameamua kujiunga na CCM.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti leo jijini Dar es Salaam katika hafla iliyondaliwa na Uongozi wa CCM Wilaya ya Ilala, wamesema kuwa sababu ya msingi iliyosababisha kuhama kumetokana na utendaji bora wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.



Wanachama hao wamebainisha kuwa wamejipanga vyema kufanya kazi na Serikali na awamu ya tano kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala pamoja na kuhakikisha wanavibomoa vyama vinavyopinga maendeleo.



Akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala Mwita Waitara, amesema kuwa uongozi wa Chama cha CHADEMA umekuwa  ukipinga juhudi za serikali ambazo wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo.



"Baada ya kuona yale ambayo nilitaka kuyafanya tayari CCM wanayafanya, na lengo ni kuleta maaendeleo ya wananchi, nimeona ni vizuri nikaongeza nguvu kwao ili kufanikisha mipango yangu ambayo tayari inafanyiwa kazi" amesema Mhe. Waitara.



Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanaosema watu wanaomia CCM wamenunuliwa kitu ambacho sio kweli, kwani kuhama kumetokana na kulizika na utendaji wa Rais wetu Dkt. Magufuli.


Katika hafla ya kuwatambulisha wanachama wapya wa kutoka vyama pinzani viomgozi mbalimbali wa CCM walifanikiwa kushuudia tukio hilo.

Baadhi ya viongozi hao ni  Madiwani, wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM jimbo la Ukonga, Baraza la wajumbe vijana jimbo la ukonga pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu ya mkoa.

Agosti 7 mwaka huu aiyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti kwa tiketi ya CUF, Omary Kumbilamoto alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli.

“Nimejivua uanachama wa CUF na nafasi zangu zote ndani ya chama ikiwemo ya udiwani katika kata ya Vingunguti pia unaibu meya wa manispaa na nimechukua hatua hii ili kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ninaowatumikia"
Alisema kuwa amefanya hivyo ili niendelee kutekeleza majukumu yake ipasavyo najivua ikiwemo kuunga mkono jitihada za rais Magufuli na viongozi wote Serikali kwa ujumla” amsema Kumbilamoto.
Alisema kuwa kwa sasa ataendelea na shughuli zake za kilimo mpaka pale atakapoamua kuwajulusha wananchi chama gani atachoamua kujiunga upya.

Julia 28 mwaka huu Mwanasiasa wa upinzani Mwita Waitara alitangaza kujiengua katika chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA na kujiunga na Chama tawala, CCM.

Waitara aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga lililopo Dar es salaam alifikia uamuzi huo kutokana na madai kuwa  chama alichotoka, Chadema hakina demokrasia na pia kotofautiana na mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

Alisema kuwa chama hicho kikuu cha upinzani kimeshindwa kujenga ofisi  ya kitaifa na ofisi za kanda licha ya kupokea ruzuku inayozidi milioni 200 kila mwezi.

Waitara ambaye kwenye mkutano huo aliambatana na Katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekisifia chama tawala na viongozi wake kwa kudai wanaokwenda spidi katika kuwatumikia watanzania.

"Chadema ni kampuni na sio taasisi, ukiwa nje unaweza kudhani ni makamanda kweli lakini ukiingia ukaona yanayofanyika ni shida,"amesema Waitara

Kwa mujibu wa sheria mwanasiasa huyo sasa anakuwa amejiengua katika nyadhifa zake za kisiasa ikiwemo ubunge aliopata mwaka 2015.

Baadhi ya viongozi wa chama tawala na wafuasi wao wamemiminika kwenye mitandao ya kijamii, wakipongeza uamuzi wa Waitara huku wanasiasa wa upinzani wamimshutumu kwa usaliti.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania, wanasiasa wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani wamekuwa wakijuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama tawala, kwa wanachodai kuuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages