WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali za
Mashindano makubwa ya 26 ya Kusoma na Kuhifadhi Kuruan Tukufu Duania.
Mbali na majaliwa, viongozi wengine
watakaohudhuria fainali hizo zitakazofanyika katika ukumbi wa Diamond DiamondJubilee, kesho, jijini Dar es salaam ni marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dk.
Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu Dk. Mohammed Gharib Bilal
Akizungumza jijini na waandishi wa
habari,, Mratibu wa mashindano hayo,
Sheikh Mohammed Nasoro, kutoka Taasisi ya Kuhifadhisha Kuruan TukufuTanzania
ambao ndiyo wandaaji wa mashindano hayo,
amesema jumla ya nchi18 zitashiriki.
Amezitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni
Tanzania, Saud Arabia, Mali, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Malawi, Congo
DRC, Russia, Sylia, Yemen, Malaysia,
Bangladesh, Uingereza, na Burundi.
“Washiriki wote wamewasili
nchini ambapo juzi na jana tuliwafanyia
mashindano ya mwisho ya kupata wale bora ambao wataingia katika fainali
kesho,”alisema Sheikh Nasoro.
Alisema, majaji watatoka nchi za
Uingereza, Yemen, Saud Arabia na Sudan
na tayari wamewasili nchini.
“Zawadi tutatangaza baadaye ingawa
pia fainali hizo zitakwenda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa watu mbalimbali,”alibainisha.
Katibu wa Taasisi ya Kuhifadhisha
Kuruan Tukufu Tanzania, Mohammed Ally Hassan, amewaomba watanzania kushiriki
kwa wingi kwani jambo hilo ni la kheri hasa katika kipindi hiki cha Ramadhan.
Akizungumza kwa niaba ya jopo la
majaji wa fainali hizo, Jaji Dk. Abbas Hamza kutoka nchini Sudan , amesema
wanaamini haki itatendeka na kuwataka watanzania kuhudhuria kwa wingi.
No comments:
Post a Comment