Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala akipokea kombe la Jumla ambapo manispaa hiyo wamejitwalia Ubingwa kwa kunyakua makombe saba.
Picha ikionyesha Makombe ambayo Manispaa ya Ilala wamejishindia.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Janeth Nsunza akizungumza na wanafunzi, waalimu, pamoja na Wadau walioshindiki Michezo hiyo.
Na Anna Chiganga Utouh news.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wameibuka mabingwa wa Jumla kwa Mkoa Dar Salaam katika Mashindano ya UMITASHUMTA yaliyokuwa yakifanyika katika mkoa huo ambapo yalihusisha Manispaa za Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni Pamoja na Ubungo.
Katika mashindano hayo Ilala iliweza kunyakua Makombe 7, ambapo imeongoza na Nafasi ya Pili ilichukuliwa na Kinondoni na Huku nafasi ya Tatu wakiwa ni Wilaya ya Temeke.
Akizungumza na wanafunzi wadau pamoja na walimu walioshiriki michezo ya Umintashumta wakati wa kilele cha Michezo hiyo, Kaimu katibu tawala Mkoa ambaye pia ni Afisa Elimu Taaluma katika Mkoa huo, Janeth Nsunza amesema katika kuhitimisha michezo hiyo kimkoa wameunda timu iliyoshirikisha halmashauri zote tano zitakazopambana katika Mikoa mingine ili kupata mshindi kitaifa.
Amesema licha ya Manispaa ya Ilala kushika nafasi ya kwanza ameitaka timu iliyochaguliwa ambayo ni ya Mkoa kuweza kushiriki vyema ili kuweza kuibuka mshindi wa kwanza kitaifa.
"Mwaka Jana mkoa wetu ulikuwa washindi wa 3, hivyo nahitaji timu hii ya mkoa iliyochaguliwa kutuwakilisha vyema na kuweza kushika nafasi ya kwanza"Amesema Nsunza.
Aidha amezitaka manispaa ambazo hazijapata kombe kuweza kutia bidii katika mashindano yajayo.
Pia amewaahukuru wadau walioshiriki, Maafisa elimu walimu wakuu pamoja na walimu wa michezo kushiriki vyema katika kuhamasisha na kuweza kufanikisha michezo hiyo,huku akimpongeza Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala.kwa Ushindi walioupata.
Tazama Picha za matukio mbalimbali katika Ufungaji wa Michezo ya UMITASHUMTA katika Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Uhuru Jijini hapo.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Kinondoni ambaye amekuwa Kaimu Afisa Elimu Mkoa, akitoa Utambulisho
Halmashauri ya Kinondoni
Manispaa ya Ilala
Makombe ya Manispaa ya Ilala.
Masispa ya Temeke wakiwa katika Maandamano.
Manispaa ya Ubungo.
No comments:
Post a Comment