Mfumuko wa bei wa Taifa Kwa mwezi Mei 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.6 ukilinganisha na asilimia 3.8 mwezi April 2018.
Takwimu hizo zimetolewa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo ambapo ameeleza kuwa kupungua Kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua Kwa mfumuko wa bei za bei za vyakula.
Aidha ametaja baadhi za vyakula vilivyochangia kupungua Kwa mfumuko huo kuwa ni pamoja na mahindi 10.3%,unga wa mahindi 12.5%,mtama 13.8%, unga wa mihogo 15.2%,viazi mviringo 9.0% na mihogo mibichi 12.6%.
Hata hivyo mfumuko wa bei wa nchi za Afrika Mashariki umepungua Kwa asilimia 1.7 mwezi Mei 2018 kutoka asilimia 1.8 April 2018 kwa nchi ya Uganda huku nchini Kenya ukiongezeka Kwa asilimia 3.95 mwezi Mei kutoka asilimia 3.73 April mwaka huu.
No comments:
Post a Comment