A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 10, 2018

Wolper akubali yaishe

Malkia wa filamu, Jacqueline Wolper ameamua kunyamaza na kusitisha malumbano yaliyoanza kwenye mitandao kati yake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Harmonize.

Malumbano hao yasiokuwa ya kawaida yameanza Jumanne hii baada ya Harmonize kupost list ya wanaume aliodai wamewahi kutembea na mpenzi wake huyo wazamani, Jacqueline Wolper.

Hatua hiyo ilimfanya Wolper kuibuka na kuanza kuandika mambo mbalimbali mabaya akimtuhumu muimbaji huyo wa wimbo, DM Chick, huku akidai ndiye aliyesababisha alumbane na Sarah.

Alhamisi hii Wopler aameamua kuwa mpole kwa kufunga malumbano hayo baada ya Harmonize kudai ataandaa list C ya wanaume aliotembea na mrembo huyo kutoka katika kiwanda cha filamu.

“Mungu nifundishe kunyamaza, we ndio unaujua ukweli 🙏#Najifunzakuheshimkilangaziiliyonifikishanilipo
#NdiomaanataupambanesiwezkushukaatanishushaMungupekee #jifunzekuheshimkilangaziiliyokufishaulipokamweutoteterekakwajarbulolote
#MunguwanguwaushindiwewenijbuToshaNimekukabidhiwewekilaktu🙌🙏,”

Baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii wanadai Harmonize anamchokoza Wolper ili apate kiki za project yake mpya.

Muimbaji huyo siku ya leo ameachia kolabo yake wimbo ‘Pull Up’ alioshirikishwa na Eddy Kenzo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages