A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 10, 2018

Shilole amjibu Ebitoke


 Msanii wa muziki na filamu bongo ambaye pi ni mjasiriamali, Zuwena Mohamedi maarufu kama Shilole, amejibu tuhuma za Ebitoke aliposema kuwa hamjui mlimbwende huyo kama msanii, na kusema kwamba hana shida ya kujulikana naye kwani sio level zake.

Akizungumza na www.eatv.tv, Shilole amesema kwanza hana muda wa kubishana na watu wasio na hela kama Ebitoke, na kuhusu kumjua ana imani kila siku anamtazama sebuleni kwake, na kama alisema hivyo kutafuta kiki atafute watu wa level zake kwani yeye sasa hivi hatoi kiki.

"Nina imani nyumbani kwake ananitazama kila siku na ninamuinsipire vibaya mno, wengine wanapenda wanisikie nikiongea, mi siwezi kuongea na mtu ambaye hana hela, lakini wakati huo ananijua na ananiangalia kwenye tv sebuleni kwake, mimi sitoi kiki sasa hivi, atafute wenzie ambao ni level yake”, amesema Shilole.

Shilole ni miongoni mwa wasanii wa kike waliopigana kutoka kimaisha kuanzia kufanya filamu, muziki na sasa ni mjasiriamali maarufu wa chakula hapa bongo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages