BAADHI ya wasanii wa Bongo Muvi wamemuandalia hafla fupi msanii mwenzao, Wema Sepetu, wakimpongeza kutokana na tuzo alizoshinda kwenye tuzo za sinema zetu zilizoandaliwa na Azam TV.
Wema amewashukuru sana wasanii wenzake kwa hafla hiyo na pia amesema ameyasikia maneno maneno ya baadhi ya wasnii wengine walioponda yeye kupata tuzo hizo, lakini anazichukulia kama changamoto tu kwenye maisha kwani huwezi kupendwa na kila mtu.
Aidha Wema amezungumzia uhusiano wake na Mwanamitindo, Hamisa Mobeto, ambaye awali alikuwa rafiki yake lakini baada ya kuzaa na X-wake Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, urafiki umepungua kidogo.
“Hamisa ni kama Mdogo wangu, lakini kuna wakati sijui mazoea yakizidi sana kunaleta mushkeri kidogo, kwahiyo kila mtu anatakiwa kubaki kwenye mipaka yake,” amesema Wema.
No comments:
Post a Comment