Simba wanakabidhiwa ubingwa wakiwa mjini Singida hata kabla ya kuivaa Singida katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, keshokutwa Jumamosi.
Hii inatokana na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga kufungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Kufungwa kwa Yanga kuinaifanya ibaki na pointi 48 katika nafasi ya tatu, Azam FC katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 na Simba sasa wanachukua ubingwa wakiwa na pointi 65.
Simba wanachukua ubingwa wakiwa na pointi tatu mkononi.
No comments:
Post a Comment