WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kupitia Taasisi yake ya Odo Ummy Foundation leo amegawa futari kwa taasisi za kiislamu na magereza zilizopo Jijini Tanga vyakula mbalimbali ili viweze kuwasaidia wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8
Akizungumza mara baada ya kukabidhi futari hizo mapema leo taasisi zenye wanafunzi waliotika maeneo mbalimbali na wakati mwengine wanakuwa hawana uhakika wa kufutari,watu wengine wajitoleza kulea taasisi hizo pamoja na alisema ameona atoe futari hiyo kwa kila taasisi badala ya kuwaita pamoja kufuturu nao maana wengine wanaweza kushindwa kupata fursa ya kuhudhuria lakini wakikabidhiwa wanaweza kuona namna nzuri ya kuweza kuitumia wakati wa mfungo mtukufu wa ramadhani.
“Nimeona ni bora nitoe futari hii badala ya kwenda kufuturu kila mahali kwani tutakapofanya hivyo wanaweza kuja wachache na mimi kutokana na kuwa nimetoka kwenye familia ya watu wa kawaida maskini nimeona angalu hicho kidogo ambacho nimejaliwa nitoa kwa taasisi za dini na watoto kwenye mazingira magumu”Alisema.
No comments:
Post a Comment