Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wadau wa chanjo, wameanzisha chanjo mpya ya kuwakinga na Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi wasichana wenye umri wa miaka 14 kuanzia mweziApril, 2018 kwa nchi nzima.
Serikali imeamua kuanza kutoa chanjo hii kwasababu saratani ya mlango wa kizazi inaongoza kwa kuua wanawake wengi ukilinganisha na saratani nyingine.
Akizungumza leo katika ufunguzi wa Chanjo hiyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amesema inachangiwa na vitu vingi na lengo hasa la chanjo hiyo ni kuwakinga Mabinti wadogo wanaopatwa na Ugonjwa huo.
"Lengo hasa la kuanzisha chanjo hii ni kuwakingamabinti zet u n a mad har a y ana yow e z a kuwapata ambayo yanasababisha vifo kwa wanawake, na hivy o, u anz is hw aj i w a ch anj o hii utaboresha Afya ya Wakazi wa mkoa wetu na Watanzania kwa u jumla"Amesema.
Amesema walengwa kwa mwaka huu ni wasichana wote wanaotimiza miak a 14, ambapo kwa mkoa huo wanatarajia kuchanja wasichana wasiopungua elfu ishirini na nn e n a tis in i na s aba i f ik apo Disemba 2018( 24, 097) .
Aidha ameeleza Sababu za Saratani ya mlango wa kizazi ambapo inaonekana kuwa inachangiwa na vitu vingi ikiwemo k ua nz a k uj amian a k ati ka um ri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuwa na ndoa za mitala, kuzaa w atot o w e ng i, na uv utaj i w a sigara na kusema kuwa Dalili za saratani ya mlango wa kizazi mara nyingi hujitokeza baada ya kuanza kusambaa.
"Dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuishiwa damu , f igo k us hi ndw a ku f any a kazi, kupatwa na fistula, na uvimbe wa tezi"Amesisitiza.
Ameendelea kusema kuwa "Tunapaswa kujua namna ya kujikinga na Saratani ya mlango wa k iz azi.
Nj ia yak w anz a ni k upa ta chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi, kutokufanya ngono k ati ka um ri m dog o, ku ep uk a kubeba mimba katika umri mdogo, kuwa na mwenzi mmoja mw amin if u, ku tum ia ko nd omu n a kuepuka uvutaji wa sigara.
Njia ya pili niKufanya uchunguzi wa ki na il i ku bai ni d alil i za aw al i na kupata matibabu stahiki mapema. Na njia ya tatu, kupata matiba bu ma alum k w a mtu am bay e tayari amepata saratani ya mlango wa kizazi"
Ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jin s ia, Wa ze e n a Wa toto k w a kushirikiana na wadau mbalimbabali katika jitihada za kubores ha af y a ya ma binti Nchini ikiwemo kupunguza vifo vitokanavyo na saratanikwa kuanzisha chanjo dhidi ya u go njw a wa saratani ya mlango wa kizazi.
"Tunafahamu kuna changamoto nyingi katika mapambano dhidi ya saratani.
Tunajaribu kukabiliana na changamoto zilizopo, ili k us im amia na k ub or e sh a Af y a ya Wakazi wa Mkoa wetu wa Dar es salaam" Amesema Lyaniva.
Amewataka Wazazi pamoja na Walezi, kuhakikisha kuwa watoto ambao wamefikisha umri wa miaka 14 wanaenda katika vituo vya kutolea huduma za chanjo ikiwemo vituo vya Afya , s hule na baadhi ya maeneo katika jamii yaliyopangwa kutumika kwa huduma ya utoaji wa chan jo kam a huduma y a mkoba ( out rech services).
Aidha amewahakikishia wananchi kuwa chanjo zinazotolewa katika vituo v yetu ni salama, hutolewa na wataalamu wenye uzoefu mkubwa waliobobea katika fanihii kwamuda mrefu.
No comments:
Post a Comment