Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando, akizungumza na waandishi wa habari wanafuzni pamoja na walimu nkatika hafla hiyo.
Serikali imetoa wito kwa wazazi wote nchini kuchangia Chakula shuleni ili kupunguza utoro na kusukuma wanafunzi kuhudhuria vipndi vya masomo kwa wakati.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya elimu kwa shule za msingi, katibu tawala Mkoa Theresia Mbando amesema kuwa wazazi wana wajibu wa kuchangia kwani itasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi ili tuendelee kuongoza kitaifa.
"Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake, ili kufikia malengo ya kupate matokeo mazuri lazima wanafunzi waandaliwe kupenda shule na jamii yote iwajibika katika elimu" amesema Mbando.
Aidha walimu wa shule zote nchini lazima wafundishe kwa kufuata mitaala bora iliyokidhi vigezo ilioyowekwa na serikali ili kutatua changamoto ndogondogo zinazojitokeza katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake kaimu afisa elimu Mkoa Janeth Msunza amesema kuwa kupitia maadhimisho hayo ya wiki ya elimu kimkoa, wanafunzi wanapata fursa ya kushindana kimasomo pia kufahamu wajibu na nafasi yao kielimu
"Walimu na wazazi lazima wafuate waraka wa elimu uliotolewa na seikali ambao unaelezea namna bora ya kuchangia michango ya na utoaji wa chakula ili kuweza kuinua sekta hii ambapo itasaidia kupata matokeo chanya" amesema Msunza.
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment