Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa
Mabenki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), leo
(25/05/2018) imezindua mpango wa hatifungani wa miaka mitano kwenye Soko la
Hisa (DSE). Uzinduzi huo ulifanywa na
Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo Bw. Ammish Owusu-Amoah jijini Dar es Salaam ulishuhudiwa na
wawekezaji pamoja na wadau mbalimbali toka sekta za fedha, nyumba na sekta
nyingine.
Uzinduzi wa utoaji wa dhamana
ya TMRC ulifanyika baada ya TMRC kupokea kibali kwa ajili programu ya utoaji wa
dhamana ya miaka 5 yenye thamani ya Sh Bilioni 120. Mpango huo ulipata kibali
kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji (CMSA) pamoja na Soko la Hisa (DSE).
Kampuni hiyo ya TMRC itaorodheshwa kwenye DSE.
Aidha, CMSA na DSE, zilijumuisha
kuendelea kwa TMRC kutoa dhamana ya ushirika wake ambayo itakuwa kiasi cha Sh Bilioni
12. Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Oscar Mgaya alisema "tumepokea vibali
vyote muhimu na tunatarajia kwenda kwenye Soko la Hisa kwa mara ya kwanza hivi
karibuni".
TMRC ni taasisi maalum ya sekta
binafsi ya Fedha ambayo hutoa fedha za muda mrefu kwa taasisi za fedha kwa
madhumuni ya mikopo ya nyumba. Taasisi hii ina lengo la kuunga mkono taasisi za
kifedha kutoa mikopo ya nyumbaya muda mrefu ambayo husaidia kushusha marejesho
ya kila mwezi na kuwezesha wateja wengi kumudu. Aina hii ya kukopesha pia
inajulikana kama mikopo ya jumla.
TMRC inatafuta
fedha ili kusaidia shughuli zake za mikopo ya nyumba. "Ilifikiriwa tangu
mwanzo kwamba TMRC itapata fedha kutoka kwenye masoko ya mitaji kupitia utoaji
wa dhamana kati ya vyanzo vingine" alisema Mgaya. "Ilikuwa tu suala
la muda na sasa ni wakati mzuri kwa sababu riba za soko zimekua zikishuka" aliongeza Mgaya.
No comments:
Post a Comment