Na James Timber, Musoma
Wauguzi nchini wamekula kiapo cha ahadi kumhudumia mgonjwa yeyote pasipo ubaguzi na utunzaji wa siri za wateja wao kama kanuni na taratibu zao zielekezavyo.
Akiongea katika mahojiano Maalumu na Muungwana Blog baada ya kumalizika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wauuguzi Duniani Kitaifa iliyofanyika mkoani Mara katika Halmashauri ya Musoma Mjini ambapo mgeni Rasmi alikuwa Stella Ikupa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Makamu wa Rais wa Chama cha Wauguzi nchini Dk. Ibrahim Mgoo aliomba wananchi watofautishe taaluma na siasa.
"Wananchi waache kujichukulia sheria mkononi kwa kuwashambulia wauguzi wakiwa katika kutekeleza majukumu yao ya kazi na kitaaluma, sambamba na viongozi wa serikali wasiofuata taratibu za utumishi wa umma, ukosefu au upungufu wa vitendea kazi isiwe sababu ya kuwashambulia wauuguzi kwa maneno na vichapo, alieleza.
Dk. Mgoo alieleza baadhi ya changamoto ni kama kutosajiliwa kuwa na chama chao cha wafanyakazi, uhaba wa wauuguzi, kutopandishwa madaraja ya mishahara kwa wakati na ucheleweshwaji wa malipo ya sare ya wauuguzi.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo "Wauguzi ni Sauti iyongozayo Afya ni Haki ya Binadamu" huadhimishwa Duniani Kote Kumkumbuka Muasisi wa Taaluma ya Uuguzi Duniani Bi. Florence Nightingale ambaye alizaliwa Mei 12, Mwaka 1820 huko nchini Italia.
No comments:
Post a Comment