A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 2, 2018

Wanafunzi 6 wa Shule moja watumbukia katika shimo la choo Kenya



Wanafunzi sita wa shule moja wa eneo la mashinani Kenay wameanguka katika shimo la choo baada ya choo hicho kuporomoka Jumatano asubuhi, vyombo vya habari nchini vinaripoti.

Leo ni siku ya kwanza ya muhula mpya katika shule ya msingi ya Kisulisuli kaika kaunti ya Nakuru mkoa wa bonde la ufa.

Taarifa zilisambaa mwendo wa saa mbili asubuhi kuwa choo katika shule hiyo kimeporomoka na wanafunzi wamezikwa ndani.

Wazazi walikimbia katika shule hiyo kwa haraka na mara moja jitihada za uokozi zilianza kwa ushirikiano wa jamii na maafisa wa uokozi, Udongo mbichi ulifukuliwa na mawe yakavunjwa kuwafikiwa na kuwaokoa wanafunzi hao sita.

Awali idadi ya watoto waliozama haikujulikana, lakini baada ya mwalimu mkuu kuwahesabu wanafunzi wote, alithibitisha kupitia vyombo vya habari nchini kwamba wote wako salama.

Choo hicho cha nje katika shule ya msingi ya Kisulisuli kiliporomoka kufuatia mvua kubwana mafuriko ambayo yamekuwa yakishuhudiwa nchini kwa wiki nne sasa, Uwanja wa michezo wa shuel hiyo pia umefurika.

Mkasa wa leo unafuatia msururu wa mikasa kama hiyo nchini Afrika kusini ambapo idara ya elimu sasa imetenga mpango maalum unaopiga marufuku vyoo vya mashimo katika shule za msingi.

Kituo kimoja cha televisheni kimemnukuu mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Kisulisuli aliyesema kuwa kati ya wanafunzi sita waliokolewa, wanne wako salama, lakini wawili walijeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages