Katibu Mkuu Tume ya utumishi wa walimu Tanzania Winfrida Rutahindurwa, amewataka walimu wakuu kusimamia taratibu na Sheria za kazi na kutoa adhabu kwa Mwalimu yeyote atakayeenda kinyume na Sheria bila kujali anauhusiano gani na kiongozi yeyote serikalini.
Ameyasema hayo leo katika MKutano wake na walimu wa Maispaa ya Ilala uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee na kuwataka walimu kufuata nidhamu shuleni na kutowachapa viboko Wanafunzi badala yake watumie mbinu nyingine walizo fundishwa ikiwemo adhabu ndogo ndogo ili kuweka ukaribu na wanafunzi na kuwafanya wasome kwa bidii.
Amewataka walimu wa kiume kuwapenda watoto wa kike, na kuacha tabia ya kuwatamani na kuwataka kimapenzi jambo linalopelekea kukatisha masomo ya mwanafunzi hiyo na hata kushindwa kufanya vizuri darasani.
"Wanafunzi wa kike wanapofikia umri wa kuvunja ungo wanabadilika wanapendeza nawaomba walimu wakiume wapendeni wanafunzi wa kike ila msiwatamani wapendeni kama watoto wenu mnavyo wapenda msiwape mimba msiwabake na kukatisha ndoto zao ukibainika adhabu ni kufukuzwa kazi hatanikikupa walimu wa kike msiwatamani wavulana " Amesema.
Kwa upande wa mavazi, amewataka walimu kuvaa nguo zenye staha na kuacha kuvaa nguo zenye picha mbaya na maandishi ya kutisha kwani litapelekea wanafunzi kushindwa kusoma na kutazama picha hizo.
"Utakuta Mwalimu amemvaa nguo yenye picha ya chui katoa Meno mnawatisha wanafunzi, mimi nakumbuka nilipo kuwa na Soma Marangu tuliandamana kwa sababu Mwalimu wetu alikuwa anavaa vibaya tuka goma kuingia darasani" Amesema.
Hatahivyo amewataka walimu kufundisha wanafunzi kwa bidii ili waweze kufaulu na kuwapa mazoezi ya mitihani ya kuwapima.
"Walimu wa Biology acheni kutumia vitabu vya Nyam bali Nyangwine ni bomu havifai kama kuna Mwalimu bado inatumia vitabu hivyo aache tabia hiyo" Amesema
Pia amewataka waalimu kuacha kukopa fedha nyingi zinazosababisha kushindwa kulipa na kuwapelekea kuweka rehani hata kadi zao za benki.
No comments:
Post a Comment