A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 23, 2018

UVCCM yasema miradi ya maendeleo Dar ipo vizuri.



Na Heri Shaaban

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam imesema miradi yote ya maendeleo iliyokuwepo katika mkoa huo ipo vizuri.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo Mussa Kilakala wakati wa Baraza la Vijana lililoandaliwa na Kamati ya UVCCM Mkoa Dar es Salaam.

"Miradi ya maendeleo ikiwemo afya,  elimu na  miundombunu katika halmashauri za mkoa huu inaendelea vizuri "alisema Kilakala.

Kilakala aliwataka wasimamizi wa miradi yote ya maendeleo iliyopo halmashauri    itunzwe vizuri waliopewa mamlaka wasimamie na kukuza uchumi.

Aidha alisema wanatarajia kutoa semina Elekezi kwa wajasiriamali walipo halmashauri tano za mkoa huo ili fedha za mikopo ziweze kutumika vizuri ziweze kusaidia vijana  wote.

 "Halmashauri zote nchini zinatakiwa kutenga asilimia 10 za mapato ya ndani kwa ajili ya mapato ya Wanawake na vijana na watu wenye ulemavu"alisema.

Alisema mikopo hiyo ni muhimu kwa kundi hilo ili liweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Pia alisema anatarajia kufanya ziara katika halmashauri hizo Kujua vijana walionufaika na mikopo hiyo.

Kwa upande mwengine aliwatoa hofu wananchi na kusema kuwa kwa sasa serikali yetu ya awamu ya tano
inakwenda vizuri nchi yetu ya Kizalendo kila Mtanzania amuunge mkono Rais John Magufuli kwa uwajibikaji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages