UONGOZI na Kamati ya Maandalizi Klabu ya Yanga SC wamefanya mabadiliko kwa kusogeza mbele tarehe ya Mkutano Mkuu wao.
Mkutano Mkuu wa klabu hiyo ulikuwa ufanyike Mei 5 mwaka huu lakini sasa unatarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu katika Bwalo la Polisi Oyestabey jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Charles Boniphase Mkwasa amesema kamati imekaa na kujadiliana, hivyo wameona wasogeze mbele tarehe ya mkutano huo kwa sababu za kimsingi zilizojitokeza.
"Tuna mechi nyingi za Ligi zitakazokuwa zinaendelea hapa katikati pamoja na hilo baadhi ya viongozi watakuwa nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza katika hatua ya makundi katika Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger, "amesema Mkwasa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makundi ya WhatsApp ya Yanga Tanzania Bakili Makele amewataka wanachama wote wa klabu hiyo nchini kulipi kadi zao.
"Ni muhimu kwa kila mwanachama kulipia kadi yake ya uanachama iwe ya Benki au ya kawaida ili auhudhurie mkutano huo ili kila mmoja apate haki yake ya kuchangia na hatimaye kuondoa changamoto zilizopo na tusonge mbele,”amesema Makele.
No comments:
Post a Comment