A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 8, 2018

Sugu Kuwasha Moto Baada ya Kutoka Gerezani

Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu'' amefunguka na kusema kuwa atawasha moto katika jiji la Mbeya Mjini pindi atakapotoka kutumikia kifungo chake cha miezi mitano jela ambapo sasa kinakwenda ukingoni.

Sugu amesema hayo kupitia kwa Mwenyekiti wa baraza la vijana la Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (BAVICHA) Taifa Patrick Ole Sosopi ambaye mwisho wa wiki iliyopita alipata fursa ya kumtembelea katika gereza la Rwanda.

"Siyo siri ni kwamba tunaamini mwezi huu watatoka wote ila Sugu anasema atawasha moto Mbeya, na kuwatumikia wananchi na kukutumikia chama mahali popote ambako chama kitamfanya aweze kwenda kwa kuwa yeye ni mjumbe wa kamati kuu, hivyo yapo mambo mengi naamini akitoka atayaeleza mwenyewe kwa undani zaidi, pia Masonga ameahidi akitoka atawaeleza wananchi ni jinsi ambavyo tunapaswa kupigania haki zetu na kuwa hatupaswi kuwa waoga nali tunapaswa kufanya harakati kwa njia nzuri na salama na kugusa maisha ya watanzania ambao tunawaongoza na kuwatetea" alisema Sosopi

Mbali na hilo Sosopi alieleza kuwa viongozi hao wametoa shukrani kubwa kwa watanzania pamoja na wanachama wa CHADEMA kwa jinsi ambavyo walikuwa wanakwenda kuwapa faraja kwa kuwaona magereza.

Hata hivyo Sosopi amedai kuwa viongozi hao mwezi huu wanaweza kutoka japo hajasema itakuwa lini na kusema kuwa watu wa magereza wao ndiyo wanajua siku gani na tarehe gani viongozi hao watatoka ndani ya mwezi huu.

"Tuwe na subira siyo kwamba ni siri lakini tuwe na subiri tunatambua kwamba viongozi wetu hawa wamebakisha muda mchache sana watatoka... ni lini nafikiri hatupo tayari kueleza hilo kwani ni mapema zaidi ila tutawaeleza tu tutakapokuwa tunaona kuna sababu ya kuwaeleza ni lini watatoka lakni tunaamini ndani ya mwezi huu watatoka kwa sababu ni wakati muafaka, kama unavyojua sisi si wasemaji wa Magereza kwamba tunajua wanatoka lini, ila tunachojua watatoka ndani ya mwezi huu" alisisitiza Sosopi

Februari 26, 2018 Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi kwa jina maarufu Sugu na mwenzake Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walihukumiwa kwenda jela kwa miezi mitano kwa kosa la kumkashfu Rais John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages