Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imemtaka Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye kuandika barua ya maelezo ya matatizo ya jimbo lake kuhusiana na kufungwa kwa vituo vya afya kama ilivyoagizwa hapo awali ili tatizo hilo lisiweze kujirudia.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 08, 2018 na Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kandege Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 24 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge Nape Nnauye ambaye aliyeuliza serikali ni kwanini isichukue hatua za dharula kwa zahanati zilizofungwa katika maeneo yote jimboni mwake.
"Tukiwa hapa Bungeni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika alitoa taarifa kwamba kama yupo Mbunge yeyote na wa eneo lolote ambalo tunalazimika kufunga Zahanati au Kituo cha Afya kutokana na ukosefu wa watoa huduma aandika barua na kumpelekea Mkuchika ili tatizo hilo lisiwe kutokea. Naomba kama Mhe. Nape hakuwepo siku hiyo basi atumie fursa hiyo ili hicho anachokisema kisiweze kutokea", amesema Kandege.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Josephat Kandege amempongeza Mbunge Nape Nnauye kwa jimbo lake kwa kuweza kujengwa vituo vingi vinavyotoa huduma za afya.
No comments:
Post a Comment