A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, May 11, 2018

Sugu Atabiriwa Urais Bungeni


Mbunge wa Mikumi ambaye pia ni msanii Prof. Jay, amemtabiria Mbunge na Msanii mwenzake Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, kuja kuchukua wadhifa mkubwa wa nchi, mara baada ya kuachiwa huru kutoka kifungoni.

Prof. Jay ametoa utabiri huo Bungeni leo alipokuwa akichangia hoja, na kusema kwamba kitendo cha Sugu kufungwa gerezani kimemuongezea ujasiri, ambao utakuwa chachu ya kuweza kuwa Rais wa Tanzania hapo baadaye.

“Natoa pongezi kubwa sana kwa pacha wangu Sugu kwa kuhitimu mafunzo huko ndani ambayo yameongeza ujasiri na CV yake ya kisiasa na natumaini sasa hivi hatakuwa rais wa Mbeya bali anakwenda katika mchakato wa kuwa Rais wa Tanzania huko mbeleni.”, amesema Prof. Jay.

Sugu ameachiwa huru hapo jana kutoka gereza la Ruanda mkoani Mbeya alikokuwa amefungwa kutumikia miezi mitano jela, sambamba na mwenzake Katibu wa Chadema kanda ya Nyasa Emmanuel Maosnga, kwa makosa ya kutoa lugha chafu na kejeli

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages