A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, May 11, 2018

Shilole awafungukia wanaume wanaoazima nguo

Msanii wa BongoFleva na mjasiliamali nchini Tanzania, Zuwena Mohamedy maarufu kama 'Shishi Babe' amefunguka na kuwataka baadhi ya wanaume wenye tabia ya kuvaliana au kuazima nguo hasa za ndani kuacha mara moja kwa kuwa jambo hilo sio zuri.

Shishi Babe ametoa kauli hiyo siku za hivi karibuni wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha DADAZ kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi 6:00 mchana baada ya kuulizwa swali na waongozaji wa kipindi hicho kuwa ni kwa nini watu wanapenda kuazima vitu na kushindwa kurudisha.

"Zamani wanawake walikuwa wanaongoza kwa kuazimana lakini hivi sasa mpaka wanaume wanaazimana nguo mpaka za ndani. Mimi sipendi kabisa masuala ya kuazimana vitu haswa nguo kama wanavyofanya wadada wengine wa mjini na kama mtu akija kuniazima kitu kwangu huwa naangalia na muda mwingine naigawa kabisa na siwezi kuichukua tena", amesema Shishi Babe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages