A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 10, 2018

Siwezi Kupata Mtoto Sasa Hivi Labda Miaka 5au 6 Inayokuja:Lulu Diva


Mwanadada Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa hatokaa kubadilisha msimamao wake wa kupata mtoto sasa hivi kwa sababu hana  mpango wa kupata mtoto kwa sasa kama ambavyo alishasema tangu hapo awali,

Kuna kipindi cha hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa Lulu Diva alishapata mtoto huku awali lakini mtoto huyo amemuacha kwa mama yake na kwamba hataki watu wajue kama anamtoto, kitu ambacho Lulu Diva mwenyewe alikanusha na kusema kuwa amekuwa akikaa na watoto wa ndugu zake wengi kwahiyo hana mtoto wala hategemei kupata mtoto kwa sasa.

"Kama mtoto nilishasemaga kuwa siwezi kupata mtoto sasa hivi labda miaka 5 au 6 inayokuja not now, maana sio kitu cha kukimbilia."

Akiongea na waandishi wa habari alipokuwa katika ufunguzi wa car wash ya Perfect Chrispin, Lulu Diva anasema kuwa kwa sasa amejikita kuwekeza zaidi katika kilimo kwa sababu kuna mashambe mengi ya mama yake ambayo ameachiwa na marehemu baba yake kwaio akiwa kama mtoto mkubwa kwenye familia yao ameona ni bora kuyafanyia kazi mashamba hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages