TIMU ya Simba imechapa Ndanda FC inayopambana isishuke daraja, bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufikisha pointi 65 katika msimamo wa ligi, lakini kinachowavutia watu zaidi ni kwamba timu hii ndiyo pekee katika msimamo huo ambao haijapoteza mechi.
Yanga imeshapigwa mechi mbili, Azam imepigwa tatu. Sasa Yanga ambayo ipo katika nafasi ya tatu, inahitaji zaidi ya miujiza ili iweze kuikamata Simba. Imeachwa pointi 17 ikiwa imebakiza mechi sita ambazo zina jumla ya pointi 18. Si rahisi.
Na hata kama Simba ikipoteza mechi zote zilizobaki, halafu Yanga ikashinda zote, zikalingana pointi, bado itawalazimu Yanga wafanye miujiza ya kufunga angalau zaidi ya mabao matatu katika kila mechi, kitu ambazo ni nadra kutokea.
Hakuna ubishi tena kwamba Simba imefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18 labda itokee miujiza isiyo ya kawaida. Kimahesabu, Simba wanatakiwa kupata sare mbili tu katika mechi zake tatu zilizobaki, hivyo unaweza kusema ina asilimia 98 za ubingwa.
Na Simba hii itakosaje hizo sare mbili katika mechi zake tatu zilizobaki dhidi ya Singida, Kagera na Majimaji wakati hadi sasa imecheza jumla ya mechi 27 kwenye Ligi Kuu Bara bila kupoteza hata moja?
(PICHA: RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS)
No comments:
Post a Comment