Serikali imesema ipo tayari kulipa deni la mikopo inayodaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mara tu baada ya Kanuni za kuunganisha mifuko ya Hifadhi za Jamii kupelekwa kwa wadau ili kupata maoni yao na hatimaye zianze kutumika.
Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Tumbe,Rashid Ali Abdallah aliyetaka kujua ni lini Serikali itarejesha mikopo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
“Mwaka 2016, Serikali ilifanya uhakiki wa deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii linalotokana na mikopo ya uwekezaji kwenye miradi mbalimbali ili kuandaa utaratibu wa malipo ambapo jumla ya deni lililowasilishwa Serikalini kwa ajili ya uhakiki kwa mifuko yote ni shilingi trilioni 2.1 na deni lililokubalika baada ya uhakiki ni shilingi trilioni 1.2”, alisisitiza Dkt. Kijaji.
Akifafanua, Dkt. Kijaji alisema kuwa baada ya uhakiki kukamilika, Serikali ilianza kuandaa utaratibu wa kulipa deni hilo kwa kutumia hati fungani maalum zilizotarajiwa kuiva katika kipindi cha kati ya miaka mitatu hadi 20.
No comments:
Post a Comment