Bi Edith Max akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Hi ndio nyumba ambayo tayari imeanza kubomolewa na taasisi hiyo.
Bi Edith akionyesha nyumba hiyo namba 868 iliyopo Mfaume Road Upanga mashariki
Mwenekiti wa mtaa huo Abdulkarim Gulam Shmbe akizungumza na waandishi wa habari.
Familiya moja iliyokuwa ikiishi Mfaume Road, Kata ya Upanga Mashariki, jijini Dar es Salaam wamepaza sauti na kilio kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mkuu wa mkoa wa Mkoa huo RC.Paul Makonda kuwasaidia kupata haki yao amabayo inaonekana kuporwa kwa nguvu na taasisi ya Khoja Shia ambayo ni ya kidini kwa kudai kuwa walinunua nyumba hiyo.
Amesema walibaini udanganyifu katika unaofanywa na Benki hiyo kwani kila wakitaka kulipa deni wanaambiwa wasubiri na baada ya hapo waligushi vyeti vya mirathi feki na hakuna mwanafamilia yeyote alietambulika katika mirathi hiyo.
Aidha Bi. Max amesema Familia ili fungua Mirathi yake tarehe 17 Januari katika Mahakama ya mwanzo Kinondoni na Msimamizi wa Mirathi hiyo Max Edmund Kafipa.
Amwsema awali suala hili walilipeleka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Kampeni yake ya kuwa sikiliza walidhulumiwa nyumba, viwanja na Mashamba ambapo walifika katika ofisi hizo January 30, mwaka huu.ambapo pande zote ziliitwa na kujadiliana kwa wanasheria na maamuzi yao yanatarajiwa kutolewa tarehe 7 May 2018.
Ameendelea kusema kufuatia kuendelea kwa kesi hiyo taasisi hiyo ilifika na kubomoa nyumba hiyo jambo ambalo ni kinyume na sheria na walipobaini waliomba zuio na wakabata barua ya kuzuia kuvunjwa kwa nyumba hiyo.
"Hii taasisi ambayo ni ya kidini wanasema ni watetezi wa wanyonge lakini si kweli kwani wamekuja na wanavunja nyumba yangu hii usiku wakidai kuwa wamenunua na ni Mali yao tulipewa zuio la kutovunja lakini wanakuja kuvunja hata Jana usiku walikuja kuvunja kwa siri Mimi nalia naomba Rais wangu na Mkuu wa mkoa mnisikie kilio changu nipate haki yangu" Amesema Bi Edith.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Abdulkarum Gulam Shambe, amesema ni kweli kuwa jambo hilo lipo na mgogoro huo kati yao na benki na kwamba taarifa za kuvunjwa kwa nyumba hiyo alipata baada ya kuanza kuvunja ndipo walipopeleka taarifa hizo kwake.
No comments:
Post a Comment