RC MAKONDA akizungumza na wananchi wa Kilungule Mbagala Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. RC Makonda akikagua moja ya nyumba iliyoanza kutitia
Hizi ni baadhi ya Nyumba zilizotitia na kubomoka kutokana na Mafuriko
RC Makonda akizungumza na wakazi wa Kilungule.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amewahimiza Wananchi wote waliojenga kwenye maeneo hatatishi ikiwemo mabonde na sehemu zenye miinuko kuondoka ili kujikinga uharibifu wa Mali na vifo visivyokuwa na ulazima.
Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua uharibifu wa nyumba zilizovunjika eneo la Kingugi kwa Mnyani Kata ya Kilungule baada ya wakazi kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
Aidha amewaagiza Wenyeviti wote wa mitaa kuainisha nyumba zilizojengwa kwenye maeneo hatarishi ambapo amewataka kutoruhisu watu kujenga maeneo ya mabondeni.
Katika kutafuta mwarobaini wa tatizo la wananchi waishio mabondeni Makonda ameandaa mkutano wa wananchi wote waishio maeneo ya mabondeni kwaajili suluhisho la kudumu.
Katika ziara alizofanya amejionea nyumba nyingi zikiwa zimejengwa kwenye maeneo yasiyo rasmi kiasi kwamba hata ikitokea janga la moto inakuwa vigumu Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika na hata mgonjwa akizidiwa gafla ni vigumu kuwahishwa hospitali jambo ambalo ni hatari kwa usalama.

No comments:
Post a Comment