MAKOCHA wa zamani wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog na Mganda, Jackson Mayanja, wametuma salamu za kuipongeza timu hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Simba ambayo imechukua ubingwa wa ligi hiyo msimu huu ikiwa chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre, ilianza kunolewa na makocha hao kabla ya kuondolewa mwishoni mwa mwaka jana.
Mayanja ambaye alikuwa kocha msaidizi, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka Simba, kisha akafuata Omog aliyekuwa kocha mkuu.
Akizungumza na Championi Jumatatu moja kwa moja kutoka Cameroon, Omog alisema: “Naipongeza Simba kwa ubingwa iliouchukua, ni jambo zuri kuona imekuwa bingwa msimu huu ambapo mimi nilianza kuinoa kama kocha mkuu. Hivi sasa nipo zangu huku nyumbani na familia yangu.”
Naye Mayanja akiwa zake Uganda, amesema: “Naipongeza Simba kwa kuchukua ubingwa msimu huu, walistahili kweli kufanya hivyo kutokana na mikakati ilivyokuwa tangu awali.”
Huu ni ubingwa wa 19 kwa Simba tangu kuanza kwa ligi hiyo ambapo Yanga inaongoza kwa kulibeba taji hilo baada.
No comments:
Post a Comment