A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 14, 2018

Mwafrika ateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia

Leo May 14, 2018 Makhtar Diop, raia wa Senegal ameteuliwa kuwa makamu wa rais wa Benki ya Dunia (WB) atakayekuwa anasimamia miundombinu.
Diop alitangazwa kushika nafasi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa taasisi hiyo muhimu duniani.
Taarifa iliyotolewa na benki hiyo inasema Diop anayaanza majukumu hayo mapya baada ya kuwa Makamu wa Rais anayesimamia Afrika katika miaka sita iliyopita akifanikisha kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya Dola 70 bilioni za Marekani.
Ndani ya miaka hiyo sita, Diop alisimamia miundombinu ya usafiri na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), nishati na madini, fedha na ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPP).
‘Katika majukumu yake mapya, Diop atasimamia ufadhili wa miundombinu ya fedha katika ufanikishaji wa maendeleo endelevu hivyo kupunguza tofauti iliyopo kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Uteuzi wa Diop anayetajwa kuwa miongoni mwa Waafrika 100 wenye ushawishi zaidi duniani utaanza July 1.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages