A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 14, 2018

BREAKING NEWS: Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameachiwa kutoka gerezani


Leo May 14, 2018 Taarifa iliyotufikia muda huu ni kumhusu Muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu, amebadilishiwa adhabu kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania na sasa atatumikia kifungo cha nje.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.

Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ambaye baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa upande wa mshtakiwa alitoa hukumu.

Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mpenzi wake.


Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje, amesema Lulu amebadilishiwa adhabu hiyo kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ambapo atatumikia kifungo cha nje.

Amesema pia kwamba, msanii huyo aliachiwa tangu juzi Jumamosi Mei 12, huku akisisitiza kuwa si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, ambayo kisheria inaitwa ‘community service.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages