A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, May 19, 2018

Mtoto wa Rais Ramaphosa aoa kwa ng’ombe 100

Wakati Uingereza leo May 19, 2018 wakishuhudia ndoa ya kifalme kati ya Prince Harry na aliyekuwa muigizaji wa Marekani, Meghan Markle, nchini Uganda kutakuwa na tukio la aina yake la kuhuisha ndoa kati ya mtoto wa kwanza wa Rais wa Afrika Kusini aitwaye Andile Ramaphosa na mpwa wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Amama Mbabazi.

Mbabazi aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Uganda kwa kipindi cha miaka tisa na baadaye kuwa mmoja kati ya wapinzani wakuu wa Serikali, akigombea urais dhidi ya Rais Yoweri Museveni akichuana pia na Dr. Kizza Besigye, katika uchaguzi wa mwaka 2016.

Andile, mtoto wa Rais Cyril Ramaphosa ameingia jana mchana nchini Uganda akiwa na msafara wake kwa lengo la kumuoa Bridget Birungi Rwakairu ambaye alikuwa mpenzi wake wa siku nyingi, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor.

Kijana huyo ameongozana na mama yake, wajomba zake pamoja na shangazi zake.

Sherehe ya kitamaduni inayofahamika kwa jina la ‘Okhushaba’, ikiwa na maana ya ‘kuomba’ itafanyika katika makazi binafsi ya Amama yaliyoko jijini Kampala.

Katika sherehe hizo, familia za pande mbili za wachumba wanaotarajia kufunga ndoa hutambulishwa rasmi na baadaye kufanya makubaliano ya mahari ambayo imetajwa kuwa ni ng’ombe 100 ambao itatolewa na familia ya bwana harusi mtarajiwa.

“Kwa mujibu wa mila na desturi zetu, sherehe ya ‘Okhusaba’ itafanyika Mei 19, katika eneo la Nyanyi Gardens ambalo ni eneo la Mheshimiwa Amama Mbabazi,” inaeleza taarifa iliyotolewa na familia ya Amama.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages