Msanii wa Bongo Fleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba
amesema sababu kubwa ya yeye kukataa kumsaini mkongwe Abby Skillz katika
'label' yake ya 'King's Music' ni kutokana na mtu huyo hapo awali ndiye
aliyemsaidia kuingia kwenye muziki hivyo isingekuwa heshima kufanya
hivyo.
Alikiba ametoa ufafanuzi huo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi
cha Planet Bongo ndani ya Heshima ya BongoFleva inayorushwa mubashara
kupitia EATV baada ya msanii huyo kuiambia EATV kuwa yupo chini ya
King's Music lakini kwa bahati mbaya muda ulipokwenda kidogo
zikajitokeza taarifa kuwa hayupo tena ndani ya label hiyo jambo ambalo
liliwachanganya watu na kutaka kujua ukweli wa jambo hilo ukoje.
"kiukweli niliweza kumsaini Abby Skillz kwenye label yangu ya King's
Music lakini niliona simtendei haki kwasababu aliniingiza katika 'game'
ya muziki na nikaweza kuona mwanga wa muziki wa bongo fleva kwa hivyo
nikaona ni bora Abby ajitegeme yeye kama yeye", amesema Alikiba.
Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema "kwasababu ukiwepo katika
label ya King's Music lazima kuna asilimia pia zinakuwa zinatoka nini.
Mimi sikutaka kumfanyia hivyo Abby, nilichokuwa nataka afanye muziki
wake, ajisaidie yeye mwenyewe lakini tutakuwa naye pamoja katika
kumsaidia kazi zake".
Alikiba amesema aliamua kuchukua maamuzi hayo kwa kuwa hakuona sawa
kummiliki mtu ambaye aliweza kumsaidia kuingia katika muziki ambapo
mpaka sasa anajulikana na kila mtu.
No comments:
Post a Comment