Benki ya
Biashara ya Mkombozi PLC, ni miongoni mwa benki ya biashara hapa
nchini
inayokua kwa kasi. Imetashatangaza kutoa gawio la faida kwa wanahisa wake
wote ifikapo
mwezi Julai mwaka huu.
Mkurugenzi
mtendaji wa benki, Ndugu George R. Shumbusho amesema bank
itafanya
malipo ya gawio kwa mujibu wa ratiba za hitaji la soko la hisa la DSM –
DSE. Na
benki inatarajia wanahisa wote kupata gawio ndai ya mwezi Julai.
Kwa mujibu
wa mkurugenzi mtendaji. Tangangazo la siku ya gawio la faida ni
tarehe 26
mwezi Mei na kufuatiwa na mauzo ya hisa yatakayokua na gawio
yatakayofanyika
kati ya tarehe 26 mwezi Mei hadi tarehe 15 mwezi Juni.
Ameyazungamza
hayo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa
benki ya
bishara ya Mkombozi, uliokutanisha zaidi ya wanahisa 100. Na kuongeza
kuwa mauzo
ya hisa yasiyokuwa na gawio yataanza kuuzwa kuanzia tarehe 16
mwezi juni.
“kitabu cha
wanahisa cha malipo ya marejesho kitafungwa rasmi mnamo tarehe 20
mwezi Juni,
na kufunguliwa upya tarehe 21 mwezi Juni mwaka huu”. Alisema.
Mkurugenzi
mtendaji ameongeza kuwa baada ya hatua zote hizi kukamilika
Wanahisa
wanatarajiwa kuanza kupokea gawio la faida kuanzia tarehe 6 mwezi
Julai mwaka
huu.
“Gawio la
hisa kwa mwanachama litagawiwa moja kwa moja kupitia akaunti ya
benki ya
mteja. Pia kupitia huduma za pesa kwa njia ya simu kama vile m-pesa,
airtel pesa
na tigo pesa” alisema ndugu Shumbusho. Shumbusho ameongeza kuwa
kwa mwaka
huu gawio limeongezeka hadi kufikia shilingi 25 kwa kila hisa kutoka
shilingi 20
ilivyokua mwaka jana.
Upanuzi wa
huduma za kisasa zinazofanywa na MKCB PLC zimefanya urahisi wa
utoaji wa
huduma kwa wateja. Hii imesaidia banki kutoa huduma zinazoridhisha
wateja na
kwa ufanisi wenye kutatua changamoto za huduma za fedha kwa mtu
mmoja mmoja,
kampuni na wafanyabiashara.
Hadi
ilivyofika tarehe 31 mwezi Disemba 2007, jumla ya thamani ya mali za benki
zimeongezeka
na kufikia shilingi bilioni 150.67 ukilinganisha na ilivyokuwa shilingi
bilioni
128.17 mwaka 2016. Kisi hicho cha fedha ni sawa na ongezeko la 17.6%.
Amana za wateja pia zimengezeka
na kufikia shilingi bilioni 121.12 hadi mwishoni.
No comments:
Post a Comment