FANALI za Mashindano makubwa
ya 19 ya Kusoma na Kuhifadhi Kuruan
Tukufu Afrika zimetikisa dunia
ambapo ambapo Rais Dk. John Magufuli
jana amelazimika kumpigia simu Waziri Mkuu Kassim, Majaliwa
kutaka mwakani aweze kuhudhuria fainali hizo.
Akihutubia maelfu ya watu ndani ya
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, jana, Waziri Mkuu Majaliwa alisema, akiwa
uwanjani hapo, Rais Dk. Magufuli alimpigia simu na kumuuliza masuala mbalimbali
kuhusu mashindano hayo.
"Wakati niko hapa mbele
nimepokea simu kutoka kwa Rais Dk. Magufuli akaniuliza hao wote walio jaa
uwanja ni waislam? Nikamwambia ndiyo ila naamini kuna ambao si waislaam
pia.Akauli za tena nawewe ni mgenirasmi miaka miwili mfululizo? Nika sema
ndiyo, akasema mwakani mimi nitakuwa mgeni,”alisema Majaliwa taarifa ilyoamsha shangwe kubwa uwanjani
hapo.
Mbali na suala hilo Majaliwa alisema, kutokana na kufana kwa mashindano hayo
ambayo huandaliwa na Taasisi ya Al-Hikma Foundation ya jijini Dar es Salaam,
Waziri wa Dini wa Saud Arabia ambaye
alikuwa ni mgeni mwarikwa Dk. Saleh
Mohammed Abdul Azizi Al Sheikh , ameahidi kujenga Chuo Kikuu cha Kiislamu hapa nchini.
“Waziri wa Dini wa Saudi Arabia amevutiwa na fainali hizi hivyo ameahidi
kutujengea chuo kikuu cha kiislamu hapa nchini,”alisema Majaliwa.
Alisema, pia Waziri huyo
ameahidi mwakani atamleta Imamu wa Msikiti wa Macca kushuhudia fainali
hizo hivyo katika fainali hizo imamu
huyo atakuwa pamoja na Rais Dk. Magufuli.
“Yaani mpaka ninarengwarengwa na
machozi ya furaha kuonyesha ni namna
gani mashindano haya yanavyoliletea sifa
taifa letu.Kitendo cha rais kukubari
kuhudhuria mwakani inatupa faraja kubwa,”alisema Majaliwa.
Katika hotuba yake, Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka taasisi za dini kuunga
mkono juhudi za serikali katika kuendeleza elimu nchini.
“Ni vema kila mmoja kuwekeza kwenye elimu.Hatuwezi kufikia malengo bila kuwekeza katika elimu.
Rai yangu ni kwa taasisi za dini
kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali kwa
kujenga shule na vituo vya elimu ili tuweze kuifikisha nchi yetu katika
uchumi wa kati,”alisema Majaliwa.
Alisema, serikali inatambua na kuthamini mchango wa
taasisiza kidini na itaendelea kutoa
ushirikiano kwa taasisi hizo.
Pia, Majaliwa aliwataka watanzania
kutunza amani iliyopo na kuona viongozi
wa dini kujiepusha na kauli zinazoweza kusababisha uhasama.
“Mtakubaliana
nami kuwa amani ya nchi yetu, ndiyo inatufanya tutembee vifua mbele dhidi ya
wenzetu, ni neema kubwa ambayo kila muumini anapaswa kuilinda kwani ikipotea
hata mkusanyiko wetu huu wa leo si rahisi kufanyika mahali kama hapa,” alisema.
Aliongeza; “Tuko hapa kwa sababu tuna amani, kama Serikali
isingekuwa inashirikisha Watanzania wote kulinda amani, basi tusingeweza
kukutanika hapa. Kuna nchi 18 ziko hapa, na watu wake wamekuja hapa uwanjani
kwa kuwa wana uhakika na amani tuliyonayo sisi Watanzania,” alisema.
Waziri
Mkuu Majaliwa alibainisha , nchi ambazo
amani imetoweka, watu wanalazimika kufanya shughuli za ibada majumbani au kwa
kujificha.
“Wenzetu hao, hawapati fursa adhimu kama hii
ya kujumuika pamoja na majirani, ndugu, jamaa na marafiki kusikiliza na
kufurahia kisomo chakuruan au kufanya shughuli nyingine za kiuchumi na
kijamii,” aliongeza.
Aliwataka Watanzania
waendelee kubeza na kupuuza kauli za walio wachache ambao kwao kuzungumzia
amani ni kujipendekeza kwa Serikali.
“Watu
hao wamesahau kwamba tofauti katika Uislamu hazikuanza leo, lakini tofauti hizo
hazikuwa sababu ya wema waliotangulia kuacha kuheshimiana na kushirikiana,”
alisisitiza.
Katika
mashindano hayo kijana wa Kitanzania, Shujaa Suleiman (23) ameibuka kidedea na kitita cha
sh. milioni 15 kwenye kundi la washiriki
wa juzuu 30.
Shujaa
mkazi wa Morogoro, amejishindia pia kompyuta mpakato ambapo kampuni ya City Property Internationala Limited imeahidi kumpa kiwanja chenye hati eneo la Kigamboni ,
jijini Dar es Salaam .
Mshindi wa pili
kwenye kundi hilo la juzuu 30 ni Ahmed Noor wa Sudan ambaye ameshinda sh.
Miliini 12.5 na kopmpyuta mpakato
akifuatiwa na Muzamil Awadh Mohamed wa Sudan alijishindia sh. milion 7.5
pamoja na lkompyuta mpakato.
Mshindi wa nne ni
Abdulally Mohammed wa Kenya aliyepata
zawadi ya sh. Milioni 5.7na wa tano ni
Ibrahim Maazur kutoka Niger, aliyepata sh. Milioni 3.4.
Washindi hao wote watano walipewa zawadi ya
kwenda hijja na Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dk. Saleh Ally Sheikh.
Washiriki wengine
kwenye kundi la juzuu 30 walitoka nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji Djibouti,
Kenya, Ethiopia, Congo DRC, Nigeria, Ghana na Afrika Kusini.
Washiriki
wengine waliopewa zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi
watatu), Juzuu tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20
(washindi watatu).
Viongozi
wengine waliohudhuria mashindano hayo ni Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya
nne, Dk. Mohammed Gharib Billal, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na
mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kutoka Saudi Arabia, Comoro,
Oman, Uturuki, Kenya, Msumbiji na Nigeria, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania,
Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally na Rais wa taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Sharif
Abdilkadir Al-Ahdal.
Waziri
Mkuu amemtaka Sheikh Nurdin Mohammed Ahmad (maarufu kama Sheikh Kishki)
akaonane na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi
ili atoe maamuzi ya kiwanja chao kilichopo eneo la Matumbi ambacho mwaka jana
aliagiza kifuatiliwe taratibu zake na kisha wapatiwe.
“Kuhusiana
na suala la kiwanja mlichosema, mamlaka ya awali ni Manispaa ya Temeke na
ilishakamilisha taratibu zote za kisheria, ikapeleka kwa Afisa Ardhi wa Mkoa
kuona kama limepita kwenye vikao vyote ndipo wanaenda wizarani kupata kibali.
Hakuna sababu ya wizara kuikatalia manispaa huku eneo lenyewe likiwa kwenye
ramani kuu ya manispaa yenyewe, nenda mumuone Waziri mwenye dhamana, awape
ardhi,” alisema.
Waziri
Mkuu amefikia hatua hiyo baada ya kupewa taarifa akiwa jukwaani kwamba taasisi
ya Al-Hikma iliwasiliana na Manispaa ya Temeke, hadi mkoani wakapewa barua
zinaonyesha eneo liko sawa lakini walipofika wizarani wamekwamishwa na Afisa
mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Mama Mpetula.
Juni 11, mwaka jana katika mashindanio
ya 18, taasisi ya Al-Hikma waliomba wapatiwe kiwanja na.118 kwenye kitalu E
kilichoshikamana na kiwanja na. 117 chenye shule yao ya Al-Hikma Girls iliyoko
Temeke ili waweze kujenga zahana.
Matukio katika picha
No comments:
Post a Comment