Mbunge wa
Viti Maalum (Chadema), Jesca Kishoa amelazwa hospitali ya Bunge jijini
Dodoma baada ya kupata ajali ya gari leo asubuhi Mei 11, 2018 wakati
akienda bungeni.
“Hapa nimelazwa hospitali ya Bunge, nasikia maumivu katika mguu wa kulia lakini naendelea vizuri.
“Nimechomwa
sindano ya kutuliza maumivu na ninaendelea vyema,” amesema Kishoa mke
wa mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David kafulila
Kuhusu
mazingira ya ajali, Kishoa amesema; “katika mataa ya pale Area D, taa
zilivyoruhusu, yule wa mbele yangu hakuwa ameonyesha kama atakata kona,
sasa alivyokata kwa ghafla, mimi kufunga breki kwa nguvu ikafeli,
nikaigonga kwa nyuma.a
No comments:
Post a Comment