Naibu waziri mkuu wa Uturuki Recep Akdağ amesema kuwa Israel na Misri hazitoi ruhusa kwa mashirika ya Uturuki yanayohusika na kuwasafirisha majeruhi Uturuki kwa lengo la kupewa matibabu kaada ya kujeruhiwa na jeshi la Israel katika maandamano.
Naibu waziri mkuu wa Uturuki akiwa katika ziara Cyprus Kaskazini amekemea mwenendo wa Israel ambao ni wa kigaidi ukiungwa mkono na Marekani dhidi ya waislamu wa Palestina.
Akizungumzia kuhusu maafa katika maandamano na majeruhi, naibu waziri mkuu wa Uturuki amesema kuwa Uturuki inaitaji kutoa matibabu kwa wapalestina waliojeruhiwa.
Akdağ amesema kuwa ndege za AFAD ambalo ni shirika la kutoa misaada katika matukio ya dharura zimekataliwa na Israel na Misri.
No comments:
Post a Comment