Msanii mkongwe kwenye game ya bongo fleva na anayeheshimika na wengi, Juma Kassim Nature au Juma Natere, amemtaka msanii Young Tuso kuwa makini na kauli zake zenye kuleta dharau, kwani zinaweza zikampa madhara.
Akizungumza na www.eatv.tv, Juma Nature amesema kwamba yeye kuitwa Mfalme wa Temeke sio yeye aliyeanzisha bali ni raia wanaomkubali, hivyo msanii huyo ambaye pia anatokea Temeke, awe makini kwani inaweza ikamtokea puani.
“Hakuna ambacho anaweza akafanya kikanifanya nionekane mimi miyeyusho, kwanza anatokea wapi? we muache atajua anachokitaka atakipata, mimi sijawahi kujisifia wala sijawahi kujiita mfalme wala rais, raia wenyewe ndio wananiita mimi, nadhani hapo atakuwa amewatukana raia wenyewe, sasa awe makini sana katika maneno anayozungumza, asije siku akaenda kwenye tamasha halafu akapata madhara, vitu vingine vinakuwa havisemwagi”, amesema Juma Nature.
Hapo Jana Young Tuso amesikika akisema kwamba Juma Nature hana sifa za kuwa Mfalme wa Temeke bali yeye ndiye, kwani muda wote aliokaa kwenye game ameshindwa kujitengenezea heshima ya kuwa na hadi ya urais wa temeke kwa upande wa burudani.
No comments:
Post a Comment