Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Mhe. Zainab Vullu amewataka Wanawake Wajasiriamali Wilayani Kisarawe kuanzisha Mtandao maalumu wa kibiashara utakaowawezesha kutengeneza na kuuza bidhaa zao ili kujikwamua kiuchumi na kuenda sambamba na kaulimbiu ya Rais Magufuli ya Uchumi wa viwanda.
Mhe. Vullu ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Ujasiriamali Wilaya ya Kisarawe ambapo amewahimiza wanawake kutumia vizuri mikopo wanayopata kwenye kujiendeleza kwenye *shughuli za ujasiriamali zitakazoweza kuwaingizia *kipato badala ya kuendekeza kununua *mavazi* na kutunzana katika *sherehe.*
Aidha Mhe. Vullu amesema Elimu ya ujasiriamali waliyoipata iwe ni njia bora ya kuwawezesha kupiga hatua kiuchumi pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya mikopo.
“Msishindane kuvaa au kutuza fedha katika sherehe, rejesheni mikopo kwa wakati ili iwanufaishe wengine”. alisema Mhe. Vullu.
Hata hivyo Mhe. Vullu amewataka wanawake kuachana na wivu usiokuwa namaana bali wawe na wivu wa kimaendeleo hususan utengenezaji wa bidhaa bora zinazoweza kuhimili ushindani katika soko.
Pamoja na hayo Mhe. Vullu amewasihi wajasiriamali kuepuka propaganda za kisisa katika shughuli za maendeleo kwakuwa hata Rais Dk. John Magufuli* ameshaeleza wazi kuwa maendeleo hayana chama.
No comments:
Post a Comment