Na Heri Shaaban
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imetoa mafunzo ya walimu waliohama kutoka sekondari kwenda shule za msingi.
Mafunzo hayo ya wiki moja yameandaliwa na Idara Elimu Msingi Ilala kwa Ushirikiano wa ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa hiyo yalitolewa na wawezeshaji kutoka chuo kikuu cha Uongozi (ADEM) kilichopo Bwagamoyo mkoani pwani.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Ofisa Elimu Msingi Ilala Elzabeth Thomas,alisema Ilala imepokea majina ya Walimu waliotakiwa kuhamia jumla 70 walioripoti 80 hawakuwa tayari kuhamia shule za msingi kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo masomoni.
"Manispaa yangu imetoa mafunzo ya walimu wa sekondari ambao wamekuja msingi, lengo la mafunzo hayo kuwajengea uwezo wakiwa darasani baada kubadili ufundishaji kutoka shule za sekondari kufundisha shule za msingi "alisema Thoma.
Thomas alisema jumla ya Washiriki 65 Kati ya 70 walipata mafunzo hayo washiriki watano walishindwa kushiriki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufatilia uhamisho wa kwenda mikoani,Ugonjwa na sababu mbalimbali.
Mafunzo waliopewa na wawezeshaji ni ya kusoma kuandika na kuhesabu (KKK) katika mtaala ulioboreshwa kwa kutambua umuhimu wa mafunzo hayo wameweza kujifunza ushauri na unaishi, uchambuzi wa mtaala, uchambuzi wa mihtasari na shughuli za kutendwa na mwalimu,miongozo ya kufundishia, upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi, na utunzaji wa kumbukumbu za maendeleo ya mwanafunzi.
Aidha alisema pia walimu watatu ambao wametoka mikoani waliomba kuhamia sekondari Ilala wameripoti shule za msingi.
"Ofisi yangu kwa ushirikiano wa mkurugenzi mara baada kupokea walimu hao ambao wametoka kufundisha wanafunzi Wakubwa Idara ya Elimu msingi ikaona ni vyema yafanyike mafunzo kwa walimu hao ili waweze kutekeleza majukumu yao wakiwa shule za msingi na malipo yao tayari yametengenzwa na baadhi yao wamepokea kupitia benki zao"alisema.
Kwa upande wake mgeni rasmi Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam,Hamisi Lissu aliwataka Maofisa Elimu kuwapa fursa walimu kwani fursa zipo nyingi wadau wanawekeza shule za serikali.
Amezitaka manispaa zingine kuiga Ilala ambayo imefungua njia na kuwataka wakaguzi wa mkoa huo kufuata maelekezo na kuwashauri walimu.
Aliwataka walimu hao kusimamia misingi ya kazi zao bado ni Watumishi wa serikali
na fursa zikitokea wawapewa kipaumbele.
No comments:
Post a Comment