Klabu ya soka ya Simba imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Majimaji FC kwenye mchezo wa kufunga msimu wa ligi kuu msimu wa 2017/18 ambapo bao la Majimaji limefungwa na mshambuliaji aliyesajiliwa Simba SC Marcel Kaheza.
Mchezo huo ambao umemalizika jioni hii kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea, umeshuhudia Majimaji ikishuka daraja kutoka ligi kuu hadi ligi daraja la kwanza msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi ya 15 ikiwa na alama 25.
Kwa mujibu wa Simba tayari wameshafikia makubaliano a Kaheza ambaye alifunga bao dakika ya 5 ya mchezo, hivyo ni mchezaji halali wa timu hiyo kuanzia msimu ujao. Kaheza amemaliza msimu huu wa ligi akiwa na mabao 14 sawa na nahodha wa Simba John Bocco.
Simba imeshindwa kuwatoa kimasomaso mashabiki wake baada ya kufungwa na Kagera katika mechi ya kukabidhiwa ubingwa wiki iliyopita huku leo ikitoa sare na Haruna Niyonzima akifuata nyayo za Okwi baada ya kukosa penati.
Mbali na usajili wa Marcel Kaheza, Simba pia imeriptiwa kumalizana na nyota wa Lipuli FC, Adam Salamba ambaye naye amefanya vizuri msimu akiwa na vilabu vya Stand United mzunguko wa kwanza na Lipuli FC mzunguko wa pili.
No comments:
Post a Comment