MSANII wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya maarufu kwa jina la ‘Keisha’ ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (NEC) leo, Jumatatu, Mei 28, 2018.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kufuatia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho uliofanyika leo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Keisha ambaye aliwahi kutamba kwa ngoma yake ya uvuymilivu na nyingine, aliwapi pia kuwania Ubunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Dodoma na kushinda katika kura za maoni.
Kabla ya uteuzi huo wa leo, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.
No comments:
Post a Comment