Mama Mzazi wa Muigizaji Steven Kanumba ameupongeza uamuzi wa serikali wa kupitia mikataba ya wasanii ambayo inaonekana kuwa na dalili za unyonyaji.
Amesema kuwa hatua hiyo ni nzuri na muhimu kwake kwani amekuwa akiona kazi za mwanae kila siku mitaani lakini yeye hakuna anachonufaika nacho.
“Kwangu mimi ni faraja, namshukuru Waziri Mwakyembe kwa kuliona hilo. Kwa mfano mwanangu Steven Kanumba, movie zake naziona lakini mama yake ni masikini wanaofaidi ni wengine, sasa kupitia hilo tamko la serikali nasema asante Mungu,” amesema.
“Mimi ni staa nisiye na hela, kazi za mwanangu naziona tu mtaani lakini mimi ni maskini,” Mama Kanumba ameiambia Clouds TV.
Wiki iyopitia Bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/19, Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe alisema ameunda kamati ya wanasheria ya kuchunguza mikataba ya kibiashara waliyoingia marehemu Steven Kanumba na Mzee Majuto.
No comments:
Post a Comment