MASHINDANO ya ngumi kombe la Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita yamemalizika jana huku mabingwa watetezi ambao ni mabondia wa JKT waliibuka kidedea na hivyo kuchukua kombe kwa mara ya pili mfululizo.
Mpambano huyo wa aina yake ulimalizika jana katika uwanja wa ndani wa Taifa ambapo Meya Mwita alikabizi zawadi kwa mshindi wa kwanza ambayo ni Makao makuu ya JKT, iliyopata pointi 10.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni timu ya mkoa wa Dar es Salaam ( mzizima) chini ya Kocha Haji Fera ambapo walipata pointi nane, huku mshindi wa tatu ikiwa ni Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Awali Meya Mwita alisema kuwa michezo ni jambo muhimu kutokana na kwamba huwezesha vibaya kupata ajira, kuwaweka pamoja na kwamba katika uongozi wake jijini hapa atahakikisha mchezo wangumi unapewa kipaumbele.
Meya Mwita alifafanua kuwa kwakipindi kirefu mchezo huo ulisahaulika na kwamba jiji limeanza kujenga kituo ambacho kitatumika kwa ajili ya mashindano hayo.
"Michezo ni ajira, michezo ni burudani, utakumbuka juzi hapa tumefanya vibaya kwenye jumuiya ya madola, mtakubaliana na mimi kwamba mchezo huu wa ngumi ulisahaulika, lakini uliwahi kutuletea sifa kubwa katika nchi yetu.
Sasa nijukumu letu kama viongozi, kuungana na wadau wamichezo kufanya maandalizi ya kutosha ili turudi kwenye mstari tuliokuwa mara ya kwanza"alisema Meya Mwita.
Hata hivyo Meya Mwita aliwapongeza mabodia walioshiriki kwenye mpambano huo nakuahidi kuwa atatua changamoto zinazo wakabili sambamba na kuhakikisha kuwa wanashiriki kwenye mashindano nje ya nchi.
Mwishoo.
Imetolewa leo Mei 26 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.
Maelezo ya picha.
Pix1. Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimkabizi mshindi wa kwanza ambaye ametoka Makao makuu ya JKT kombe la ngumi la Mstahiki Meya wa jiji.
Pix 2. Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa neno la pongezi kwa mabondia walioshinda mpambano huo hapo jana.
Pix 3. Mashabiki kutoka makao makuu ya JKT wakishangilia ushindi baada ya kukabiziwa kombe na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
No comments:
Post a Comment