Malkia
wa filamu, Jacqueline Wolper ameamua kunyamaza na kusitisha malumbano
yaliyoanza kwenye mitandao kati yake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani,
Harmonize.
Malumbano
hao yasiokuwa ya kawaida yameanza Jumanne hii baada ya Harmonize kupost
list ya wanaume aliodai wamewahi kutembea na mpenzi wake huyo wazamani,
Jacqueline Wolper.
Hatua
hiyo ilimfanya Wolper kuibuka na kuanza kuandika mambo mbalimbali
mabaya akimtuhumu muimbaji huyo wa wimbo, DM Chick, huku akidai ndiye
aliyesababisha alumbane na Sarah.
Alhamisi
hii Wolper aameamua kuwa mpole kwa kufunga malumbano hayo baada ya
Harmonize kudai ataandaa list C ya wanaume aliotembea na mrembo huyo
kutoka katika kiwanda cha filamu.
“Mungu
nifundishe kunyamaza, we ndio unaujua ukweli
🙏#Najifunzakuheshimkilangaziiliyonifikishanilipo
#NdiomaanataupambanesiwezkushukaatanishushaMungupekee
#jifunzekuheshimkilangaziiliyokufishaulipokamweutoteterekakwajarbulolote
#MunguwanguwaushindiwewenijbuToshaNimekukabidhiwewekilaktu🙌🙏,”
Baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii wanadai Harmonize anamchokoza Wolper ili apate kiki za project yake mpya.
Muimbaji huyo siku ya leo ameachia kolabo yake ya wimbo ‘Pull Up’ akiwa ameshirikiana na Eddy Kenzo
No comments:
Post a Comment