A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 7, 2018

Hiki ndicho alichokisema Jaji Mkuu juu ya mlundikano wa kesi Mahakamani


Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahimu Juma leo May 7, 2018 amefungua mafunzo elekezi kwa majaji wapya 14 wa Mahakama Kuu nchini yakiwa na lengo la kuwataka wafanye kazi kwa umakini.

Jaji Prof Juma amezindua mafunzo hayo ya wiki 3, katika Kituo cha Mahakama cha Mafunzo ya Uongozi kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Amesema kuwa Majaji wanatakiwa kutambua kadri wananchi wanavyozitambua haki zao, mlundikano wa kesi unaweza kuongezeka lakini hiyo isiwe kigezo cha wao kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi ya kusikiliza mashauri yao na kuyatolea maamuzi kwa wakati.

Akizungumzia mlundikano unaosababishwa na upungufu wa majaji, Jaji Prof Juma amewataka majaji kutumia muda wao vizuri na kujitahidi kuamua kesi ambazo zinaweza kutolewa uamuzi mapema na kumalizika

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages