Serikali ya Zimbabwe imetoa ruhusa kisheria bangi kulimwa kama zao jingine la chakula au biashara.
Ruhusa hiyo imetolewa ili zao hilo litumike kwaajili ya sababu za matibabu. Kwa watakaotaka kulima zao hilo, watapewa leseni ya miaka mitano kwaajili ya kumiliki, kusafirisha na kuuza bangi na bidhaa zake zilizokaushwa.
Zimbabwe ndio nchi ya pili Afrika kufanya jambo hili baada ya Lesotho kuwa ya kwanza kugawa leseni za kufanya kilimo hicho mwezi September mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment