A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, April 29, 2018

Wilaya ya Kigamboni yazindua chanjo ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi



Na Heri Shaaban

MKUU WA Wilaya ya Kigamboni Hashimu Mgandwila amezindua semina ya kutoa elimu
Ya kuhamasisha Watendaji,Wenyeviti wa Mtaa, na Viongozi wa Dini kuhusiana na uhamasishaji wa Chanjo ya saratani ya mlango wa shingo ya uzazi.

Mgandilwa alifungua semina hiyo Dar es Salaam jana kwa ajili ya utoaji elimu kwa   hiyo ili wakahamasishe wananchi waweze kushiriki chanjo hiyo ambayo inazinduliwa leo (Jumatatu April 30)

"Naomba msipotoshe umma katika chanjo hii aizui mtu kuzaa
Na chanjo hii itawahusu kuanzia miaka saba hadi 14"alisema Mgandilwa

Alisema kila jambo linapoanza lazima liwe na changamoto
Ndio akalazimiika kutoa elimu hiyo kwa wadau kwani chanjo hiyo aina madhara kwa binadam.

Aliwataka viongozi wa dini,Wenyeviti wa Mtaa na Watendaji na viongozi wa siasa waliopata elimu hiyo wawe chachu kwa wengine.

Alisema saratani ya shingo ya uzazi ni hatari gonjwa la kwanza saratani ya matiti linafuata ili ambayo yanasababisha kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na uvutaji sigara  kunapelekea kushambulia kibofu na figo kuferi.

Aidha alisema katika wilaya hiyo kutakuwa na vituo vya chanjo 113 shule 67 na vituo 23  vya kutembea.

Kwa upande wake Meya wa Kigamboni Muhamad Hoja alisema elimu hiyo waliopata wataenda kuhamasisha umma ili kufanikisha zoezi hilo la serikali.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa Kigamboni
Zacharia Mkundi.alisema atawafikishia elimu hiyo Wenyeviti wenzake ili waungane katika kampeni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages