Rc Makonda na Rais wa shirika la KOICA Madam,Bi. Mi- Kyung Lee wakiwa katikawodi ya wazazi katika hospital hiyo.
wa shirika la KOICA Madam,Bi. Mi- Kyung Lee(kushoto) akiwasalimia baadhi ya kina mama waliojifungua katika Hospitali hiyo .
Moja ya Gari la kubeba wagonjwa (ambulance)/ambapo magari mawili yamezinduliwa rasmi leo katika Hospitali hiyo
Rc Makonda na Rais wa shirika la KOICA Madam,Bi. Mi- Kyung Lee wakiwa wamembebe Mtoto aliyezaliwa katika Hospitali hiyo.
Rais wa Shirika la Misaada la Korea Kusini KOICA Bi. Mi- Kyung Lee amezindua Hospital i ya Uzazi na Mtoto Chanika iliyojengwa kwa jitiada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambapo aliwatafuta wafadhili hao.
Ujenzi wa Hospital hiyo ya kisasa umegarimu zaidi Shillingi Billion 9.8 ambapo ndani kuna vyumba vya kisasa vya Upasuaji, vyumba vya Madaktari, Maabara,Chumba cha Mionzi, wodi ya wazazi,wodi ya watoto njiti, Theater, vyumba vya kujifungulia, ICU, Vyoo vya kisasa pamoja na nyumba za Familia 28 za madaktari ambapo ndani ya nyumba hizo kuna kila kitu.
Rais wa KOICA Bi.Mi-Kyung Lee amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo huku akipongeza Tanzania kwa kudumisha amani tofauti na Mataifa mengine.
Amesema Tanzania ni nchi ilibarikiwa kuwa na Vivutio mbalimbali ikiwemo mlima Kilimanjaro pamoja na Mbuga za wanyama ambapo watu wa Korea kusini watashirikiana zaidi hasa kufanya utalii katika vivutio hivyo na kuahidi kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na Tanzania katika kuendeleza maendeleo.
Kwa Upande wake Rc Makonda amesema aliamua kutafuta wafadhili wa kujenga Hospital hiyo baada ya kuona kilio cha kinamama waliokuwa wakipoteza maisha na watoto baada ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.
Aidha amemuomba Rais wa KOICA kumjengea Hospital nyingine mbili kwenye Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni ili kusaidia maboresho ya huduma za afya na kupunguza vifo vya kina mama.
Pamoja na hayo Makonda ameshukuru serikali ya Korea kusini kwa ufadhili wa hospital hiyo yenye hadhi ya kimataifa.
Vilevile Uzinduzi wa Hospital hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa magari mawili ya kisasa ya wagonjwa (ambulance) ambapo zizatumika katika Hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment